WAZIRI AAGIZA MSIGWA AKAMATWE POPOTE ALIPO!

Posted on by ERICK MWEMUTSI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumhoji Mbunge wa Iringa Mjini, Mch Peter Msigwa, kuhusiana na tukio la kupotea kwa Mdude Nyagali.

Msigwa amedai kuwa Mdude ametekwa jambo ambalo Masauni amesema Msigwa akamtwe ili akasaidie uplelezi huenda anafahamu zaidi kuhusu tukio hilo.

“Tumekwenda Kituo cha Polisi kuelezea kutoweka kwa Mdude Nyagali, Polisi wamesema si wao na wamekataa kufungua jalada, kabla ya kutekwa pia alitoa taarifa ya kufuatiliwa na watu lakini Polisi walikataa kufungua jalada,” amsema Msigwa.

“Mbunge Msigwa amesema Mdude CHADEMA ametekwa, ukweli wa mtu huyu hakuonekana na ukisema ametekwa inamaana unajua na bila shaka Msigwa ana taarifa hizo na nilielekeze Polisi wamtafute Msigwa ili awasaidie,” amesema Massauni.

About the Author

Leave A Response