MC PILIPILI AKAMATWA KWA MAKOSA YA MTANDAO

Posted on by ERICK MWEMUTSI

EEMMANUEL MATHIAS,  almaarufu ‘MC Pilipili’,  anashikiliwa katika kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama jijini Dar tangu tarehe 2 Mei, 2019 kwa kosa la kutumia mtandao wa YouTube bila kujisajili na inadaiwa huenda akafikishwa mahakamani leo.

Aidha, watu wengine mashuhuri  waliowahi kukamatwa kwa kukiuka kanuni za maudhui ya mtandaoni ni Soudy Brown, Shaffih Dauda, Maua Sama, mpiga picha Mx Carter na MC Luvanda.

Kanuni hizi zinazotajwa kuwa ni tishio kwa uhuru wa kujieleza nchini, zimepewa jina la Kanuni za Maudhui ya Mtandao za Mwaka 2018 (Electronic and Postal Communications (Online Content) Regulations 2018).

About the Author

Leave A Response