WOLPER: NDOA YA HARMONIZE INAWEZA KUNIPA PRESHA

Posted on by ERICK MWEMUTSI

MSANII wa Filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper amedai kuwa ndoa ya mpenzi wake wa zamani, Rajab Khan ‘Harmonize’ inaweza kumpa presha iwapo itakuwa na mbembwe nyingi zitakazomgusa. 

Wolper alisema hayo hivi karibuni alipokuwa kwenye uzinduzi wa kiwanja kipya cha Juice Kingdom kilichopo Masaki jijini Dar jirani na Maisha Club ya zamani.

“Sijazipata habari za Harmonize kumvalisha pete ya uchumba Sara ila ikifanyika ndoa huenda nikapata presha, itategemea ndoa hiyo itafungwa vipi na yatafanyika mambo gani kama ni ya kuniumiza au ya kawaida kawaida,” alisema Wolper.

About the Author

Leave A Response