MDUDE CHADEMA APATIKANA AKIWA KATIKA HALI MBAYA‬

Posted on by ERICK MWEMUTSI

SAA  chache baada ya mawakili watatu kuwafungulia maofisa wa polisi na vikosi vya usalama kuhusu madai ya kutekwa nyara na kuzuiliwa kinyume na sheria kwa mfanyabiashara na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mdude Nyagali ‘Mdude Chadema’,  amepatikana ametupwa katika Kijiji cha Makwenje, kata ya Inyala mkoani Mbeya, akiwa hai usiku wa kuamkia leo.

Mdude anadaiwa alichukuliwa na watu wasiojulikana akiwa ofisini kwake Vwawa, Mbozi mkoani Songwe siku nne zilizopita‬.

Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Masonga,  amesema: “Mdude amepatikana katika Kata ya Inyala Mkoani Mbeya, usiku akiwa katika hali mbaya ingawa anajitambua na anazungumza kwa mbali, amepigwa sana na amevimba, amekutwa na kadi ya chama chake (Chadema) na kitambulisho cha mpiga kura.”

About the Author

Leave A Response