SERIKALI YAFUTA MKATABA NA KAMPUNI YA KUNUNUA KOROSHO

Posted on by ERICK MWEMUTSI

SERIKALI imeufuta mkataba ilioingia na kampuni ya Kenya ya Indo Power Solutions Ltd iliyopewa jukumu la kununua korosho tani 100,000.

Serikali kupitia Waziri wa Biashara, Joseph Kakunda,  imesema kampuni hiyo imeshindwa kutekeleza sehemu ya makubaliano,  hivyo mkataba umefutwa. Mkataba huo uliokuwa na thamani ya Sh. bilioni 400, ulitiwa saini Januari 30 mwaka huu.

Aidha, Februari 01, 2019, mtandao wa  JamiiForums uliibua madudu ya kampuni hiyo na kuyaanika wazi (link kwenye bio),  kitendo kilichozidi kuianika kampuni hiyo ambayo ilionekana wazi ni kampuni isiyo na uwezo iliokuwa ukijinadiwa kuwa nao.

About the Author

Leave A Response