UDA-RT YASIMAMISHA HUDUMA YA MABASI MWENDOKASI

Posted on by ERICK MWEMUTSI

KAMPUNI ya UDART imesitisha huduma ya usafiri sehemu inayopitia eneo ya Jangwani na kwenda Morocco bonde la Mkwajuni kwa muda baada ya maeneo hayo kujaa maji kutokana na mvua zinazonyesha.

Msemaji wa mabasi ya mwendo wa haraka UDART,  Deus Bugaiwa,  amesema wamelazimika kufanya hivyo kutokana na hali za kiusalama.

TAARIFA KWA UMMA

Kampuni ya UDA-RT inautaarifu umma kuwa huduma za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, imesitishwa kwa muda kati ya; Kimara – Kivukoni, Kimara – Gerezani, Morroco – Kivukoni na Morroco – Gerezan kuanzia saa 10: 30 alfajiri leo Jumatatu Mei 13, 2019, kufuatia kujaa maji katika eneo la Jangwani.

Huduma zinazotolewa sasa ni kati ya;
Kimara – Mbezi, Kimara – Magomeni Mapipa, Kimara – Morroco, Gerezani – Muhimbili, Kivukoni – Muhimbili na Gerezani – Kivukoni.

Tunaendelea kufuatilia hali ya maji katika eneo husika, maji yakipungua huduma zitarejea katika hali ya kawaida.
Tunaomba radhi kwa usumbufu unaotokana na kusitishwa kwa safari hizo.

Deus Bugaiwa
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano UDA-RT.

About the Author

Leave A Response